Kiswahili kidato cha nne: maswali mchanganyiko ya Fasihi kwa ujumla (riwaya..Ushairi..Tamthiliya..

MASWALI YA FASIHI KWA UJUMLA

Haya ni maswali ya fasihi kwa ujumla kutoka katika mitihani mbalimbali ya necta

1.Fafanua fani na maudhui ya methali zifuatazo:
(a) Mgaagaa na upwa hali wali mkavu.
(b) Asiyesikia la mkuu huvunjika guu.
(c) Mchumia juani hulia kivulini.
(d) Kipenda roho hula nyama mbichi.
(e) Haba na haba hujaza kibaba.

2.“Mwandishi wa fasihi ni mchunguzi wa jamii ambaye huyaweka wazi maovu mbalimbali”. Jadili jinsi kazi za washairi wawili kati ya hao walioorodheshwa zilivyosadifu kauli hii.

3. “Matendo yasiyo na utu hujadiliwa na wasanii”. Thibitisha kauli hii kwa kutumia riwaya mbili (2)
kati ya hizo zilizoorodheshwa.

4.Kwa kutumia tamthiliya mbili (2) kati ya hizo zilizoorodheshwa, jadili jinsi kazi za wasanii hao zilivyochangia katika ujenzi wa jamii.

5.“Ngonjera na majigambo ni vipera vya fasihi simulizi vinavyofanana kimuundo na kiuwasilishaji”. Kubali au kataa kauli hii.

6.“Mshairi ni mhakiki wa jamii”. Kwa kutumia vitabu teule viwili (2) vya ushairi ulivyosoma, jadili kauli hii.

7.“Jina la kitabu ni kivutio cha wasomaji wa riwaya”. Kwa kutumia riwaya teule mbili (2) ulizosoma linganisha majina ya vitabu jinsi yanavyosadifu yaliyomo.

7“Waandishi wengi huandika kazi zao kwa lengo la kutoa ujumbe katika jamii”. Kwa kutumia
tamthiliya mbili (2) zilizoorodheshwa, thibitisha ukweli wa kauli hii.
8. “Tenzi zina kanuni maalumu”. Tunga utenzi wenye beti tatu (3) unaohusu ugonjwa wa UKIMWI.
9. Andika methali tatu (3) zinazofanana na methali isemayo “Kata pua uunge wajihi” kisha ueleze maana na umuhimu wa methali hii katika jamii.

10.Linganisha na linganua miundo iliyotumiwa na waandishi wa diwani mbili (2) ulizosoma kati ya hizo zilizoorodheshwa.

11.Lugha anayoitumia mwandishi katika kazi yake ya fasihi ndiyo inayosaidia katika kufikisha wazo lake kwa hadhira. Kwa kutumia riwaya teule mbili (2) ulizosoma, jadili jinsi wasanii wa riwaya hizo walivyotumia kipengee cha tamathali za semi.

12.Jadili kufaulu na kutofaulu kimaudhui kwa waandishi wawili (2) wa tamthiliya teule ulizosoma.

13. Umeteuliwa kushiriki katika shindano la uandishi wa ngonjera la Afrika ya Mashariki. Tunga ngonjera yenye beti nne (4) kuhusu maandalizi ya uchaguzi wa mwaka 2010.

14.Fafanua misemo ifuatayo:
(i) Mungu si Athumani
(ii) Kata mzizi wa fitina
(iii) Mtu kidole
(iv) Kondoo si mali
(v) Kuiba kauli

15. “Kiongozi katika jamii ni nahodha ambaye hutakiwa aongoze chombo kisiende mrama.” Kwa kutumia hoja tatu (3) kutoka katika kila diwani jadili kauli hii ukitumia wasanii wawili uliowasoma.

16.Jadili jinsi fani ilivyotumika kukamilisha kazi za waandishi wawili (2) wa riwaya ulizosoma, ukizingatia mtindo na mandhari.
17.Waandishi wa tamthiliya wamemchora mwanamke katika sura tofauti. Thibitisha kauli hii kwa kutumia waandishi wawili (2) wa tamthiliya mbili (2) ulizosoma.

18.Tunga shairi la kimapokeo lenye beti nne (4) kuhusu unyanyasaji wa kijinsia.

19.Sifa muhimu mojawapo ya methali ni kujenga picha au taswira ambazo huchotwa katika mazingira yanayoizunguka jamii.” Thibitisha hoja hii kwa kutumia methali tano (5).

20.“Maelekezo yanayotolewa na msanii wa fasihi hukidhi matarajio ya jamii yake.” Kwa kutoa hoja tatu (3) kwa kila mchairi, jadili kauli hii kwa kuwatumia washairi wawili (2) kati ya walioorodheshwa.
21.“Nyimbo ni mbinu ya kifani ambayo wasanii wengi huitumia ili kufikisha ujumbe uliokusudiwa kwa hadhira.” Thibitisha usemi huu kwa kutumia waandishi wawili (2) wa riwaya kati ya waliorodheshwa.

22.Jadili jinsi wasanii wawili (2) wa tamthiliya mbili (2) ulizosoma walivyotumia mbinu ya kicheko kutoa ujumbe walioukusudia kwa jamii.

23.Eleza muundo wa soga. Tunga soga ya kusisimua kuhusu kisa cha kubuni.

24.Fafanua matatizo matano ya kuhifadhi kazi za fasihi simulizi kwenye kanda za kunasa sauti.

25.“Mshairi siku zote hukemea uonevu katika jamii.” Thibitisha kauli hii kwa kutoa hoja tatu kutoka
katika kila diwani kati ya diwani mbili ulizosoma.

26“Fasihi ni chuo cha kufundisha maisha kwa jamii husika. “Jadili ukweli wa kauli hii kwa kutoa hoja tatu kwa kila riwaya kati ya riwaya mbili ulizosoma.

27.Chagua wahusika watatu wa kike, kutoka katika kila tamthiliya kati ya tamthiliya mbili ulizosoma, kisha onesha kukubalika kwao kama kielelezo cha maisha katika jamii.
28.Tunga tenzi yenye beti tano kuhusu ongezeko la watoto wa mitaani.

29.Fafanua matatizo matano ya kuhifadhi kazi za fasihi simulizi kwenye kanda za kunasa sauti.

30.“Mshairi siku zote hukemea uonevu katika jamii.” Thibitisha kauli hii kwa kutoa hoja tatu kutoka katika kila diwani kati ya diwani mbili ulizosoma.
31.“Fasihi ni chuo cha kufundisha maisha kwa jamii husika. “Jadili ukweli wa kauli hii kwa kutoa hoja tatu kwa kila riwaya kati ya riwaya mbili ulizosoma.

32.Chagua wahusika watatu wa kike, kutoka katika kila tamthiliya kati ya tamthiliya mbili ulizosoma, kisha onesha kukubalika kwao kama kielelezo cha maisha katika jamii.

33.Tunga tenzi yenye beti tano kuhusu ongezeko la watoto wa mitaani.
34.Kutokana na mabadiliko yanayoikumba jamii, baadhi ya methali zimepitwa na wakati. Thibitisha hoja hiyo kwa kutumia methali sita.

35.“Ustadi wa msanii hudhihirishwa na fani”. Dhihirisha kauli hiyo kwa kutumia vipengele vitatu vya lugha kwa kila diwani kutoka katika diwani mbili ulizosoma.

36. Jadili kukubalika kwa wahusika wawili kama kielelezo halisi cha wanajamii kati ya Takadini, Maman’tilie na Brown Kwacha kutoka katika riwaya mbili ulizosoma. Toa hoja tatu kwa kila
mhusika.

37.“Kujenga jamii bora ni dhima ya mwandishi.” Thibitisha kauli hii kwa kutumia hoja tatu toka katika kila tamhtiliya kati ya tamthiliya mbili ulizosoma.

38.Tunga tamthiliya fupi kuhusu umuhimu wa elimu kwa vijana wa Tanzania ya leo. Tamthiliya hiyo isipungue maneno mia tatu (300).

39 Kwa kutumia mifano, fafanua dhana zifuatazo kama zinavyotumika katika fasihi:
(a) Tashibiha
(b) Takriri
(c) Sitiari
(d) Tashihisi
(e) Tanakali sauti
(f) Tasfida

40.“Mtunzi wa mashairi huibua malalamiko ya kundi la wasionacho.” Fafanua kauli hiyo kwa kutumia hoja tatu kutoka katika kila diwani kati ya diwani mbili ulizosoma.

41.“Mapenzi ya dhati huleta faraja miongoni mwa wanajamii.” Tumia hoja tatu kutoka katika kila riwaya kati ya riwaya mbili ulizosoma kuonesha jinsi wahusika wake walivyofarijika na mapenzi ya dhati.
42.Onesha kufaulu kwa dhamira za msanii kwa kutumia hoja tatu kutoka katika kila tamthiliya kati ya tamthiliya mbili ulizosoma.

43. Eleza maana ya ngano kisha tunga ngano yenye maneno yasiyopungua mia tatu (300) na yasiyozidi mia nne (400).