Kiswahili kidato cha nne: jipime kwa maswali mbalimbali ya Sarufi na matumizi ya lugha

SARUFI NA UTUMIZI WA LUGHA

Haya ni maswali mbalimbali kutoka kwenye mitihani ya taifa(necta)

1.Katika kila moja ya sentensi zifuatzo onesha kosa la kisarufi kisha andika sentensi hiyo kwa usahihi:
(a) Kiboko kinaogelea.
(b) Arusi ya kaka yenu zitakuwa Disemba 2006.
(c) Mwaka huu mvua zinanyesha sana.
(d) Tafadhali nikope shilingi elfu kumi nitakurudishia kesho.

2. Andika insha yenye maneno mia moja (100) kuhusu moja ya mada zifuatazo:
(a) Maandalizi ya uchaguzi mkuu wa Oktoba 2005.
(b) Upimaji wa virusi vya Ukimwi.
(c) Mwenda tezi na omo marejeo ngamani.

3.Tunga tungo yenye vipashio vifuatavyo
(a) Nomino + Kishazi tegemezi + Prediketa + Shamirisho.
(b) Kiima hapa + Prediketa + Chagizo.
(c) Kirai nomino + Kishazi huru + Kishazi tegemezi.


4. Eleza dhima ya kiambishi “ni” kilichopigiwa mstari katika sentensi zifuatazo:
(a) Alinisaidia.
(b) Wajumbe wapo mkutanoni.
(c) Wakubalieni.
(d) Yeye ni mvivu.
(e) Nina kalamu.

5. Bainisha kauli tano (5) za vitenzi na kila kauli itungie sentensi moja.

6. Kwa kutumia mifano ya sentensi eleza dhima tano (5) za mofimu “ku”.

7.Viambishi awali na viambishi tamati vina uwezo wa kubadili umbo na maana ya neno. Katika maneno yafuatayo eleza dhima ya kila kiambishi.
(a) Watakapotupambanisha.
(b) Sielekezi.

8.Upatanisho wa kisarufi hufanya nomino mbalimbali kuwa katika kundi moja. Fikiria nomino tano na kwa kutumia sentensi moja kwa kila nomino zipange katika makundi yake.

9.Uchanganuzi wa sentensi hufanyika hatua kwa hatua. Ukitumia hatua hizo changanua sentensi ifuatayo kwa njia ya jedwali.

(a)Wale wawili watakuwa wamepimwa virusi vya UKIMWI hivyo afya zao zitakuwa nzuri.

10.Eleza njia zilizotumika kuunda misamiati ifuatayo katika lugha ya Kiswahili.
(a) Sigara.
(b) Mwanajeshi.
(c) Kipima pembe.
(d) Pembe tatu.
(e) Mtutu.

11. “Vitenzi vifuatavyo vinatofautiana kiasili”. Toa sababu za kuthibitisha jibu lako, kisha vipange vitenzi hivyo kutegemeana na uasili wake.
(a) Lima (b) Arifu (c) Ruka (d) Sali (e) Pamoja
(f) Adhibu (g) Weka (h) Buni (i) Stahimili (j) Chambua.

12.Vitenzi vya Kiswahili vina tabia zake. Kwa kutumia mifano ya sentensi tano (5) onesha tabia tano (5) tofauti za vitenzi.

13.Kuna tofauti gani kati ya mofimu huru na mofimu tegemezi? Eleza kwa kutumia sentensi nne (4), mbili (2) kwa kila mofimu.

14. (a) Eleza maana ya vidahizo vifuatavyo:
(i) Kinyenyezi
(ii) Matandu
(iii) Matlaba
(iv) Sandali
(v) Uzimbezimbe

(b) Tunga sentensi moja (1) kwa kila kidahizo.

(c).Vitenzi vishirikishi hukamilisha ujumbe katika sentensi. Kwa kutumia mifano mitano (5) thibitisha ukweli huo.

16. Fafanua dhana ya kiunganishi huru. Kwa kutumia mifano dhihirisha tofauti kati ya kiunganishi huru
na aina nyingine ya kiunganishi.

17 (a).Eleza tofauti za msingi mbili (2) zilizopo kati ya kirai na kishazi. Toa mifano miwili kwa kila tofauti.

(b)Ni kigezo kipi kinachotumika katika kuunda ngeli za kimapokeo?Dhihirisha utumiaji wa kigezo hicho kwa kutunga sentensi tano (5) za ngeli tofauti.

19. Kwa kutoa mifano, taja matumizi matano (5) tofauti ya kiunganishi “Kwa”.

20 (a).Eleza tofauti kati ya viambishi awali na viambishi tamati. Toa maoni yako kuhusu dhana ya viambishi “kati” katika Kiswahili.

(b)“Mofimu huru zina hadhi ya neno.” Fafanua usemi huu kwa kutumia sentensi tano (5) tofauti.

(c).Tumia kiambishi “KA” kuonesha matukio kumi (10).

(d).“Kila lugha ina tabia ya kuchukua maneno kutoka lugha nyingine ili kukidhi mahitaji yake
kimsamiati.” Fafanua kauli hii ukitumia maneno kumi (10) ya Kiswahili.

(e)Yapange maneno yafuatayo kama yanavyoonekana katika kamusi, kisha eleza maana ya kila neno kwa kutoa mfano mmoja (1) wa sentensi.
(a) Falsafa (b) Barizi (c) Anuwai(d) Barubaru
(e) Kinda (f) Ajuza (g) Fanusi (h) Ghaibu
(i) Goigoi (j) Kinanda

26(a)Eleza maana ya upatanisho wa kisarufi. Fafanua jibu lako kwa kutoa mifano minne.

(b).“Misemo mingi hutumika kwa madhumuni ya kulinda heshima na kuvuta makini ya watu.” Fafanua
usemi huu kwa kutumia misemo mitano (5).

27.Kwa kutumia mifano dhahiri, fafanua dhana zifuatazo:
(a) Kiima
(b) Chagizo
(c) Shamirisho
(d) Utohoaji
(e) Urudufishaji

28. (i) “Maneno huweza kubadilika kutoka aina moja na kuwa aina nyingine.” Dhihirisha kauli hii kwa kubadili maneno yafuatayo kwa kuzingatia maelekezo yaliyo katika mabano.
(a) Mkono (badili kuwa kielezi) (f) Bisha (badili kuwa kivumishi)
(b) Kwenda (badili kuwa nomino) (g) Refu (badili kuwa kitenzi)
(c) Bora (badili kuwa kitenzi) (h) Linda (badili kuwa nomino)
(d) Ogopa (badili kuwa kivumishi) (i) Kabati (badili kuwa kielezi)
(e) Mzazi (badili kuwa kitenzi) (j) Uguza (badili kuwa nomino)

(ii).Kamusi ni muhimu kwa mtumiaji yeyote wa lugha. Taja hoja tano zinazothibitisha umuhimu huo.

(iii).Kwa kutumia mifano ya lugha ya Kiswahili, taja sababu tano za utata katika mawasiliano.

(iv).Kwa kutumia mifano, taja miundo mitano ya kirai nomino.

(v)Onesha nomino katika tungo zifuatazo kisha bainisha ni aina gani ya nomino:
(a) Hatuna budi kumshukuru Mola.
(b) Mazao yamestawi shambani.
(c) Uzalendo usisitizwe shuleni.
(d) Mpeleke mtoto ndani.
(e) Nimechoshwa na upweke.

33. Andika tungo zifuatazo kwa usahihi:
(a) Mwenyekiti alihairisha kikao.
(b) Mtoto amedumbukia shimoni.
(c) Kila mwanafunzi anatakiwa kuchangia deksi.
(d) Mama amenunua dazani ya sufuria.
(e) Mwanafunzi msafi amepewa zawadi.

34 Tambulisha viambishi vyenye dhima zilizowekwa kwenye mabano katika maneno yafuatayo:
(a) Hakukumbuka (njeo ya wakati uliopita)
(b) Wamekamatana (kauli ya kutendana)
(c) Akisema (hali ya masharti)
(d) Ananiona (kurejesha mtendwa)
(e) Tuliwashangilia (kurejesha watenda)
(f) Huimba (hali ya mazoea)
(g) Wamelima (wakati uliopita hali timilifu)
(h) Wanatucheka (urejeshi wa watendwa)
(i) Hawakusoma (ukanushi)
(j) Amenipigisha (kauli ya kutendesha)

35.Onesha maana tano za neno “kata” na kwa kila maana tunga sentensi moja.

36. “Upatanisho wa kisarufi ni kigezo kimojawapo kati ya vigezo vya kuunda ngeli za nomino.”
Thibitisha dai hilo kwa kutunga sentensi ukitumia ngeli zifuatazo:
(a) U-I
(b) LI-YA
(c) U-ZI
(d) I-ZI
(e) U-YA

37.Fafanua utata uliopo katika sentensi zifuatazo:
(a) Mama anafurahia pango.
(b) Mwalimu analima barabara.
(c) Alimpigia ngoma.
(d) Kijana amepata fomu.
(e) Baba anaunda.

38. Tumia neno “Paa” katika sentensi kuunda dhana zifuatazo:
(a) Nomino
(b) Kitenzi
(c) Kielezi
(d) Kivumishi
(e) Shamirisho

39. Bainisha mzizi wa asili kwa kila neno katika maneno yafuatayo:
(a) Anawaandikisha
(b) Mkimbizi
(c) Mlaji
(d) Muumbaji
(e) Nisingelipenda
(f) Kuburudika
(g) Sadifu
(h) Aliokota
(i) Walichopoka
(j) Kipambanuliwe

40. Vibadilishe vitenzi vifuatavyo viwe katika kauli ya kutendeka:
(a) Badili
(b) Kata
(c) Komboa
(d) Zuia
(e) Fika
(f) Zoa
(g) Jenga
(h) Remba
(i) Tumia
(j) Lima 

41. Fafanua maana ya neno “chenga” kwa kutumia sentensi tano tofauti.Kwa kuzingatia tungo ulizopewa, bainisha aina za maneno yaliyopigiwa mstari: 
(a) Juzi tulishiriki maandamano ya amani. 
(b) Kucheza kwake kunaburudisha. 
(c) Kijana mlevi amepata ajali. 
(d) Hamisi alikuwa amekwisha kwenda kulima. 
(e) Wale vikongwe wamepata msaada. 
(f) Mawazo hayo si yangu. 
(g) Sitakwenda kwake asilani! 
(h) Amekwenda kazini ijapokuwa ni mgonjwa. 
(i) Hiki kitawekwa ukumbini. 
(j) Mbuzi amekwisha kata kamba. 

42. Unganisha tungo zifuatazo kwa kutumia O-rejeshi: 
(a) Mafisadi wamekamatwa. Mafisadi wamefikishwa mahakamani. 
(b) Kitabu kimenunuliwa. Kitabu kipo kabatini. 
(c) Mfadhili amepatikana. Mfadhili mkarimu sana. 
(d) Hukumu imetolewa. Hukumu ni ya haki. 
(e) Mahali pameandaliwa. Mahali hapatoshi. 

43. Bainisha kauli zinazowakilishwa na vitenzi vilivyotumika katika sentensi zifuatazo: 
(a) Refa alichezesha mechi vizuri. 
(b) Mtoto amevunjwa mguu. 
(c) Wanafunzi wanasomeana kitabu. 
(d) Mafuta yamemwagika. 
(e) Walevi wanapigana kilabuni. 
(f) Mtoto analia sana. 
(g) Babu alisomewa kitabu. 
(h) Dada anampikia mtoto uji. 
(i) Kaka alimtuliza rafiki yake. 
(j) Gazeti linasomeka vizuri. 

44. Vishazi tegemezi hufanya kazi ya vivumishi viwapo katika tungo. Onesha ukweli wa kauli hiyo kwa 
kutumia mifano minne ya sentensi. 

             MASWALI YA FASIHI KWA UJUMLA YATAFUATIA…….