KISWAHILI KIDATO CHA 3&4:HAKIKI WA RIWAYA YA TAKADINI

RIWAYA: TAKADINI
MWANDISHI: BEN J HANSON
WACHAPISHAJI: METHEWS BOOKSTORE AND STATIONERS
MWAKA: 2004

Takadini ni kitabu kilichoandikwa na Ben J. Hanson, mmojawapo miongoni mwa waandishi mashuhuri katika nchi za Afrika. Kilitolewa mara ya kwanza huko Harare (Zimbabwe) mwaka 1997.

Hii ni kazi ya riwaya ambayo huzungumzia matukio yanayotokea katika nchi za Afrika, hasa katika nchi ya Zimbabwe, ambapo watu wenye ulemavu wa ngozi, yaani zeruzeru, walikuwa wakiuawa kwa sababu ya kuamini mila na tamaduni zilizopitwa na wakati.

Kwa sasa tafsiri yake ya Kiswahili ni miongoni mwa vitabu teule katika shule za sekondari kidato cha tatu na cha nne nchini Tanzania.

MUHTASARI WA RIWAYA
Takadini ni riwaya inayojaribu kuzungumzia matatizo ya mila na desturi yaliyopo katika jamii za Kiafrika hasa sehemu za vijijini. Mwandishi anamuonyesha mhusika mkuu Takadini aliyezaliwa na ulemavu wa ngozi jinsi anavyotengwa na watoto, watu wazima na jamii yote kwa ujumla.

Mwisho tunamuona Takadini akipendwa na msichana Shingai. Pamoja na vikwazo vingi, penzi la Shingai na Takadini halikufa. Baadae Shingai anapata mimba ya Takadini, kisha anajifungua mtoto asiye mlemavu. Hapo wana jamii wanashangazwa na kujikuta wakiamini kuwa hata mlemavu anaweza kuzaa mtoto asiyemlemavu.

MAUDHUI

DHAMIRA KUU ;UKOMBOZI

Mwandishi ameeleza kuwa ili tuweze kupata ukombozi wa kweli na kujenga jamii mpya tunapaswa kuachana na mila potofu na kukomboka kifikra na kiutamaduni.Miongoni mwa mila hizo ni mauaji kwa watu wenye ulemavu.Takadini alizaliwa sope aliamriwa auawe siku ya pili tu toka atoke tumboni mwa mamaye Sekai.

Aidha makwati anasikitika baada ya kuletewa taarifa kuwa mtoto aliyezaliwa ni sope anasema…..hilositalielewa……itakuwaje….aliuliza maswali mengi (uk 12).Bila ngozi?,Sope?ni nini ulichokileta hapa kwetu?maswali haya yanaonyesha namna walemavu wasivyothaminiwa.Suala hili lilimsononesha sana Sekai inaonyesha dhahiri mtoto sope katika jamii ya Makwati hakustahili kuishi.

DHAMIRA NDOGO NDOGO

MAPENZI
Mwandishi anaonyesha mapenzi katika sura mbili tofauti yale ya dhati na ya uongo.Mapenzi ya dhati hayachagui hali wala mali pia kabila dini wala rangi.Kila mtu ana haki ya kupendwa na kupenda

  • Mapenzi ya dhati kati ya Sekai na mwanae ,Sekai alikuwa radhi auawe ilimradi furaha yake itimie ya kubaki na mwanawe sope,hakuogopa kufa alimlinda takadini na kuamua atoroke baada ya makwati kuruhusu wazee wamwangamize
  • Mapenzi ya dhati kati ya Sekai na Tendaihawa ni marafiki wa kweli walifarijiana baada ya kuelezana matatizo yao,Tendai mke mdogo wa mtemi masasa aliyelazimishwa kuolewa na mzee wa rika la baba yake.
  • Mapenzi ya dhati kati yaMzee Chivero na Sekai,mzee Chivero alimpokea Sekai na mwanawe Takadini na kuwachukulia kama wanawe (familia yake)licha ya wanakijiji wengine kuwatenga
  • Mapenzi ya dhati baina ya Takadini na Shingai ,Shingai alimpenda Takadini licha ya kuwa na ulemavu wa ngozi (sope)pia mlemavu wa mguu (alitembea kwa msaada wa gongo)kama anavyokiri mwenyewe “huyu ndiye mwanaume ninayetaka anioe”
  • Mapenzi ya uongo ni baina ya Makwati na Takadini ,Nhamo na Shangai ,Sekai na wake wenza isipokuwa Pindai
NDOA ZA MITARA
Mwandishi ameeleza athari za ndoa za mitara kuwa ni pamoja na chuki baina ya wanawake na hivyo kusababisha migogoro ndani ya familia.Mfano Sekai anasengenywa na wake wenza wake Dedirai,na Rumbidzai na kudai ni mchawi

Aidha wake wa Mtemi Masasa wanamdharau Tendai na kuchukulia kama mtoto wao na si mke mwenzao kwa sababu ya umri wake mdogo

MILA POTOFU
Dhamira hii imetazamwa katika sura tofauti kama vile:-

Wazazi kuwachagulia watoto wao wenza (wake/waume)Tendai na Shingai wanalazimishwa kuolewa na watu wasiowataka,hii ni mila potofu zilizopitwa na wakati.

Mauaji kwa walemavu ,mwandishi anaonyesha kuwa watu wenye ulemavu hawakustahili kuishi katika himaya ya akina Makwati na mtemi Masasa na ndiyo maana kuzaliwa na kuishi kwa Takadini kulileta mzozo.

NAFASI YA MWANAMKE
Jamii nyingi za kiafrika zinamkandamiza mwanamke na kumfanya mtu duni katika Nyanja mbalimbali za maisha,kama ifuatavyo;
  • Mwanamke hana maamuzi yake binafsi,watoto wa kike hawapati haki sawa na watoto wa kiume.mfano Tendai anaonekana kutofurahishwa na tendo la kuolewa na mume mwenye umri mkubwa (mzee Masasa)alisema “ni heshima kuwa mke wa mtemi mwenye nguvu kama Masasa lakini namchukulia kama baba yangu kuliko mumewangu”…….’’(uk 47)hapa inaonyesha mwanamke hana nafasi ya kuongea kama mtu mwingine.
  • Mwanamke amechorwa kama chombo cha starehe,hili linaonyeshwa kwa mzee Makwati na Mtemi Masasa kuwa na wanawake wengi kwa ajili ya kujifurahisha na hili linajitokeza bayana pale(uk 40) aliletwa mtoto kumpa joto mzee angehisi msisimko wowote ule wa mapenzi.
  • Mwanamke anachorwa kama mwanamapinduzi ,haya yanajionyesha wazi kwa Sekai na Shingai ni wanawake walioleta mabadiliko katika jamii.mfano Sekai alikuwa wa kwanza kuvunja mila na desturi kwa kukataa Takadini asiuawe na kuamua kutorokea kijiji cha jirani pia alileta mabdiliko akiwa uhamishoni
  • Shingai naye mwanamapinduzi kwani alipingana na suala kuchaguliwa mchumba aliamini kuwa ndoa ya kweli inahusisha watu wawili waliopendana na waliochaguana alisema “ Si kwamba ninamchukia Nhamo ,la hasha isipokuwa sidhani kama nitakuwa furaha ya kuishi naye”(UK 110)mwisho mwandishi anaonyesha Shingai ameolewa na Takadini na wamezaa mtoto asiye sope.

UMOJA NA MSHIKAMANO
Umoja na mshikamano ni moja kati ya nguzo muhimu katika kuleta mabadiliko na ukombozi wa kiutamaduni,mshikamano mzuri ulionyeshwa na mzee Chivero,Tendai,mtemi Masasa ulisaidia kumlinda Takadini dhidi ya unyanyapaa na hatari ya kupoteza maisha katika mapambano yoyote yenye umoja na nguvu utengano ni udhaifu

UJASIRI
Mwandishi ameonyesha kuwa Sekai ni mwanamke jasiri aliepambana kufa na kupona kumlinda mwanae Takadini dhidi ya mila na desturi za kikatili hatima yake kuleta ukombozi katika jamii.

Shingai naye ni mwanamke aliyepambana na matatizo ya kuchaguliwa mchumba,mila zinazokandamiza wanawake.
SUALA LA MALEZI
Malezi ya watoto yanapaswa kusimamiwa kwa pamoja yaani baba na mama.Katika kitabu hiki malezi yanaonekana ya upande mmoja mfano Sekai ndio mlezi mkuu wa familia hususani malezi ya Takadini

Shingai naye anapata malezi kwa mama,shangazi na bibi hata anapokata shauri la kutorokea kwa Takadini ,anaulizwa kuwa ndivyo ulivyolelewa?mzee Nhariswa anampiga mkewe na kusema “umefanya nini wewe mwanamke tangu mwanao alivyopeleka maji kwa Sekai umefuatilia kujua anachokifanya …uliona dalili kwanini hukutafuta dawa?
UJUMBE
Walemavu wana haki sawa ya kuishi kama watu wengine hivyo wathaminiwe.

Malezi yanahusisha pande zote mbili yaani baba na mama hivyo kila mmoja awajibike.

Wanawake wawe na maamuzi katika jamii hiyo ili wasinyanyaswe

Ndoa nibaina ya watu wawili wapendanao hivyo haipaswi kuingiliwa na mtu yoyote

Umoja na mshikamano ni jambo muhimu katika ukombozi wa jamii yeyote ile.

MTAZAMO WA MWANDISHI

Mwandishi ana mtazamo wa kiyakinifu,anaona kuwa matatizo yanayotokana na mila na desturi yanaweza kukataliwa na watu wengine kwa kuchukua hatua za kujikomboa kama alivyofanya Sekai na wenzake.

MSIMAMO WA MWANDISHI

Mwandishi ana msimamo wa kimapinduzi kwani ameeleza udhaifu wa baadhi ya mila na desturi zinazokandamiza watu hivyo anataka jamii ijikomboe dhidi ya mila desturi hizo.

FALSAFA

Mwandishi anaamini kuwa binadamu wote ni sawa hata kama kuna tofauti za kimaumbile lakini kila mtu ana haki ya kuishi .

MIGOGORO

Migogoro imejitokeza sehemu mbalimbali katika riwaya hii ya TAKADINI kama ifuatavyo;

  • Mgogoro kati ya Makwati na Sekai,chanzo cha mgogoro huu ni (mila na imani potofu) baada ya Sekai kuzaa mtoto sope,mtoto huyo alipaswa auawe ,mwandishi anasema suala hili halikuungwa mkono na Sekai,suluhisho sekai aliamua kutoroka kijijini ili kunusuru maisha ya mtoto Takadini.
  • Mgogoro wa Shingai na wazazi wake,Chanzo cha mgogoro huu ni mila potofu wa kuchaguliwa mchumba ambaye ni Nhamo ambapo wazazi walikasirika hata kumtolea maneno mabaya,suluhisho ni Shingai anaamua kutorokea kwa Takadini.
  • Mgogoro kati ya Sekai na wake wenzake,chanzo cha mgogoro huu ni Makwati kuzidisha upendo kwa Sekai hivyo waliamini kuwa Sekai ni mchawi
  • Mgogoro wa nafsi huu unajitokezakwa Tendai ambaye aliozwa kwa mzee Masasa ambaye alikuwa na umri mkubwa
  • Mgogoro wa kijamii,chanzo cha mgogoro ni kuzaliwa mtoto mlemavu(sope)kulizuka mgogoro baina ya wanajamii ,wao walitaka Sekai na mtoto wake wafukuzwe.

UCHAMBUZI WA FANI NA VIPENGELE VYAKE

Fani ni ule ufundi wa kisanaa anaoutumia msanii katika kazi zake. Fani ndiyo hutupatia kile kiitwacho maudhui. Katika riwaya hii, fani imechambuliwa kama ifuatavyo:

MUUNDO
Riwaya hii imetumia muundo wa moja kwa moja. Tunamuona Sekai akijifungua mtoto sope, anatoroka na mwanaye ili kumuokoa dhidi ya watu wa jamii yake. Sekai anakwenda kuishi uhamishoni, akiwa huko, mwanaye Takadini anapata mke na mtoto.

MTINDO
Mwandishi ametumia:
Masimulizi na dayolojia
Matumizi ya nyimbo. Rumbidzai aliimba;
…Mheshimiwa wetu amemiliki mavuno,
Kwa mikono yake halisi,
Kutokana na mashamba yetu wote,
Lakini ni kipi alichoambulia kutoka ardhi hii isiyomea kitu?

MATUMIZI YA LUGHA
Mwandishi ametumia lugha rahisi inayotumika kwa watu wengi,pia ametumia tamathali za semi,nahau,misemo na mbinu nyingi za kisanaa.

MISEMO NA NAHAU

Misemo na nahau imetumika katika riwaya hii ili kuipamba kazi yake

“Habari njema kuchechemea kwa mguu mmoja lakini mbaya kukimbia kama sungura.Msemo huu unamaanisha kwamba habari njema hazienei haraka ila mbaya huenea haraka sana
Pia kuna misemo mingi kama

Pokea upewacho
Maosha ni matamu
Kanga hawezi kutua kwenye bua la mtama
Mume ni kiungo kwa mwanamke

TAMATHALI ZA SEMI

Tashibiha

Matumizi ya tashibiha yamejitokeza sehemu mbalimbali

v Giza jepesi lilibakia ukutani kama mgeni asiyekaribishwa na asiyetaka kuondoka

v Muda huenda polepole sana mithili ya mwendo wa kakakuona (UK 6)

Tashihisi

Mwandishi wa riwaya ya Takadini ametumia tashihisi sehemu mbalimbal; kama vile’

Ubongo wake uliathiriwa kwa mawazo yaliofukuza usingizi wake
Fikra zilizopingana zilijichomeka katika nafsi yake
Mwanga wa jua ungaavu za novemba uliingia ndani na kulifukuza giza totoro.
Dhihaka

Mwandishi ametumia tamathali iliyoonyesha dharau na yenye lengo la kumweka mtu katika hali duni kupita kiasi lakini kwa mbinu ya mafumbo (uk 2)

v “Naamini ulichobeba sasa ni mtoto na si dubwasha”

Haya maneno yalimlenga Sekai kwakuwa siku zote waliamini hazai Tafsida

Mwandishi ametumia tamathali hii kufichaukali wa maneno (uk 83)

v Akashambulia hata sehemu za siri (UK 17)walifanya tendo la ndoa

v Akajivuta karibu zaidi naye chini ya guza hawakuzungumza wakafanya kile ambacho kilitokea kwa asili ya maumbile ,wakakata kiu ya hisia zilizowavuta pamoja miezi mingi (uk 117)

Takriri

v Wewe ni sope,sope,sope

v Najua ,najua (UK 79)

Mdokezo

v Siku moja sijui lini ….lakini hivi (UK 75)

v Sukuma mara moja tena ….(UK 125)

v Mtu mzima kama watu wengine na ameoa

WAHUSIKA

Takadini

  • Huyu ndiye mhusika mkuu wa riwaya hii
  • Ni mtoto wa Sekai
  • Ni mlemavu wa mguu na ngozi (zeruzeru )
  • Kijana wa kiume
  • Ni mchapakazi na anayependa kujituma
  • Ni mtiifu
  • Ni jasiri
  • Ni mwathirika wa mila na desturi mbaya au zilizopitwa na wakati
  • Anafaa kuigwa na jamii
Sekai
  • Ni mhisika mkuu
  • Ni mama yake Takadini
  • Ni mke wa kwanza wa Makwati
  • Mwanamapinduzi
  • Mwathirika wa mila na desturi zilizopitwa na wakati
  • Jasiri
  • Ni mwenye huruma
  • Ni mwenye upendo
Makwati

  • Mume wa Sekai
  • Baba wa Takadini
  • Ni mkali
  • Anapendana na mke wake
  • Anashiriki mila za kale

Chivero
  • Ni mzee wa makamo
  • Ni mganga wa kienyeji
  • Mwenye upendo
  • Mwenye huruma
  • Ni mshauri mkuu wa Mtemi Masasa
  • Mpenda mabadiliko
  • Alimpokea Sekai na Takadini

Mtemi masasa
  • Mzee wa makamo
  • Mtemi wa kijiji
  • Mwenye heshima
  • Ni mpole
  • Mwenye huruma
  • Mwenye wake wanne

Shingai
  • Ni binti wa mzee Nhasriswa
  •  Mke wa takadini
  •  Ni jasiri
  • Mwanamapinduzi
  • Ni msichana mwenye msimamo
  • Mwenye mapenzi ya kweli na takadini
  • Mpenda mabadiliko
  •  Ana huruma
  •  Anafaa kuigwa

Tendai
  •    Mke mdogo wa mzee Masasa
  •    Ni mke mkarimu
  •    Mwanamapinduzi
  •    Ni mpole
  •    Rafiki kipenzi wa Sekai

Dadirai
  •       Mke wa tatu wa Makwati
  •       Ni mwenye roho mbaya
  •       Mpenda majanga
  •       Ana wivu
  •       Ana mawazo potofu

KUFAULU NA KUTOFAULU KWA MWANDISHI
KUFAULU KWA MWANDISHI KATIKA MAUDHUI
-      Ameonyesha matatizo yanayowapata watu wenye ulemavu
-      Ameonyesha sababu ya watu wenye ulemavu kutokukubalika ni mila na desturi.
-      Ametoa suluhisho la matatizo hayo kuwa ni kuachana na mila hizo.
KUFAULU KIFANI
-      Ametumia lugha inayoeleweka na ina tamathali nyingi za semi.
-      Ametumia nafsi zote tatu.
-      Ameteua jina zuri la kitabu ambalo linasadifu yaliyomo.

KUTOFAULU KIMAUDHUI

-Hajaonyesha jinsi matatizo ya mila na desturi yanavyoweza kuwaathiri walemavu wengine.

KUTOFAULU KIFANI

- Ametumia idadi kubwa ya wahusika ambao hawabebi dhamira zozote.

- Hajaonyesha watu wa jamii ya Takadini walilipokeaje suala la kijana huyo kupata mtoto asiye na  ulemavu.

JINA LA KITABU

Jina la kitabu linasadifu yaliyomo kwani walemavu wanauawa ilhari hawakupenda kuzaliwa hivyo na wala sio kosa lao bali ni mapenzi ya Mungu. Takadini yaani sisi tumekosa nini? Linaonyesha jinsi walemavu wanavyouawa pasipokuwa na hatia yoyote ile