KISWAHILI KIDATO CHA PILI: UHAKIKI WA KAZI ZA KIFASIHI SIMULIZI FASIHI SIMULIZI

Fasihi ninini?
Fasihi Simulizi ni utanzu wa fasihi ambao unawakilisha sanaa ya lugha inayopitishwa kutoka kwa kizazi hadi kizazi kwa njia ya maneno/masimulizi ya mdomo.

Kwa hiyo, fasihi simulizi ni fasihi inayotungwa au kubuniwa kichwani na kuwasilishwa kwa njia ya masimulizi ya mdomo na vitendo bila maandishi.

 Fasihi simulizi hurithiwa kutoka kizazi kimoja na kingine.
Fasihi simulizi ni fasihi ya awali zaidi, kwani ilianza wakati binadamu alipoanza kutumia lugha kama chombo cha mawasiliano katika jamii ndipo alipoanza kutumia nyimbo, methali, vitendawili n.k.

SIFA ZA FASIHI SIMULIZI


Swali: Eleza sifa za fasihi simulizi ya kiswahili
  • Hupitishwa kwa njia ya mdomo
  • Ufanisi wa sanaa katika fasihi simulizi hutegemea uwezo wa msimulizi, au wahusika
  • Masimulizi yake yanaweza kuathiriwa na mazingira, hisia na hali
  • Ni mali ya jamii. Hakuna mtu fulani anayemiliki sanaa katika fasihi simulizi.
  • Inaweza kubadilika kutoka kizazi hadi kizazi, au mazingira mbalimbali kwa sababu hutegemea kumbukumbu ya msimulizi.
  • Kuburudisha - Hufurahisha na kuchangamsha hadhira
  • Kunasihi- kutolea mawaidha na kuonyesha mwelekeo unaotarajiwa katika jamii
  • Kuelimisha watu kuhusu vitu mbalimbali hasa mazingira yao
  • Kutambulisha jamii - jamii mbalimbali husifika kutokana na sanaa zao katika fasihi simulizi kama vile nyimbo
  • Kuhifadhi na kudumisha utamaduni wa jamii
  • Kuunganisha watu - huleta watu pamoja
  • Kukuza lugha - fasihi huimarisha lugha kwa kuwa hutumia mbinu mbalimbali za lugha.
  • Kuliwaza - hutoa huzuni na kuleta matumaini.
  • Kupitisha muda - wakati mwingine fasihi simulizi hutumika kupitisha muda.
  • Msimuliaji (fanani)
  • Hadhira
  • Mandhari
  • Tukio
  • Ukweli wa mambo yanayoelezwa
  • Uhalisia wa watu, mazingira na matukio katika jamii.


 VIPENGELE VYA FASIHI SIMULIZI

Huyu ni mtendaji wa tukio la kifasihi mbele ya hadhira. Tukio laweza kuwa kutamba hadithi, kuimba wimbo au kutoa kitendawili au methali. Huyu ni muhusika anayesana kazi ya fasihi.

 Hawa ni walengwa wa kazi ya fasihi ambao husikiliza na kutazama kinachotendwa na fanani. Hadhira hushiriki kwa namna fulani kwenye kile kinachotendwa iwe ni kuitikia wimbo au kupiga makofi, kutingisha kichwa au mwili. Hadhira humsaidia fanani kujitathimini juu ya kile anachokitenda na mbinu ya utendaji anayoitumia.

Hapa ni mahali ambapo matukio ya kifasihi yanatendekea. Mandhari huweza kuwa uwanjani, kichakani, chini ya mti mkubwa au mlimani.

 Hili ni tendo au tukio linalotendwa na fanani kifasihi. Tendo hili laweza kuwa usimuliaji hadithi, vitendawili, kuimba au kutoa methali.

 TANZU NNE ZA FASIHI
UHAKIKI

Nini maana ya uhakiki wa kazi fasihi simulizi?
Uhakiki wa fasihi simulizi ni kazi au kitendo cha kutafakari, kuchambua na kufafanua kazi ya fasihi simulizi ili kuweka bayana maadili na ujumbe uliomo katika kazi ya fasihi.

MHAKIKI
Huyu ni mtu anayejishughulisha na uhakiki wa kazi za fasihi zilizotungwa na wasanii wengine wa fasihi.

VIGEZO VYA UHAKIKI
Mhakiki wa kazi za fasihi simulizi atajiuliza, je ni kweli jambo linaloelezwa linafanyika katika jamii inayozungumzwa.

Kwa mfano:
Kama mhakiki wa fasihi simulizi anahakiki ngonjera inayohusu ubakaji inabidi ajiulize je kweli kuna ubakaji katika jamii inayomzunguka.
Mhakiki wa kazi za fasihi simulizi atalingalisha Wahusika waliotumiwa, mazingira na matukio katika kazi hiyo ya fasihi simulizi na hali halisi katika jamii.

Kwa mfano: kama hadithi inahusu ulevi, mhakiki inabidi ajiulize. Je katika jamii husika tabia ya ulevi ipo.
Umuhimu wa kazi hiyo kwa jamii husika lazima uzingatiwe
Mhakiki atachunguza jambo ambalo linazungumziwa kwenye hiyo kazi ya fasihi simulizi kama lina umuhimu na kuelimisha jamii. Jambo linalozungumziwa linaweza kuwa la kweli lakini halina umuhimu kwa jamii hiyo kwa kipindi hicho.

Hili linatia ndani vipengele vyake ni muundo, matumizi ya lugha, mtindo, mandhari na wahusika.

       2 Maudhui (umbo la ndani la kazi ya fasihi)

Linatia ndani dhamira, ujumbe, mafunzo, migogoro na falsafa

UHAKIKI WA USHAIRI WA FASIHI SIMULIZI

Katika fasihi simulizi ushairi ni fungu lenye kujumuisha tungo zote zenye kutumia mapigo kwa utaratibu maalum, mapigo hayo hupangwa kwa muwala wa urari wa vina na mizani. Baadhi ya fani za ushairi huambataniswa na muziki wa ala na wakati mwingine hupata mizani yake kutokana na mipangilio ya ala.

VIPENGELE VYA FANI KATIKA USHAIRI

Mashairi yana miundo tofauti tofauti ikitegemeana na ufundi wa mshairi husika. Katika muundo tunaangalia kile kinachooneshwa kwa nje.
Kwa mfano:
Hivyo, katika mashairi tuna miundo tofauti tofauti ambayo hutumiwa kuainisha kwa mujibu wa idadi ya mistari kwenye kila ubeti muundo huu ndio unatupa mashairi ya tathnia/mistari 2 tathlitha/mistari 3 Tarbia/mistari 4 Takhmisa/mistari 5.

MTINDO

-Mashairi ya fasihi simulizi yamejengwa na mitindo mingi katika utungaji
Mtindo tunaangalia vipengele kama vifuatavyo:

-Urari wa vina pamoja na ulinganifu wa mizani au ushairi unaofuata sheria za urari wa vina na mizani ni mashairi ya kimapokeo.

Mizani…. Idadi ya silabi ambazo zipo katika kila mstari
Vina……. Silabi zenye mlio unaofanana

-Mtindo wa Pindu ambapo silabi mbili (2) za mwisho wa mstari hurudiwa rudiwa mara kadhaa, Kwa mfano kama mstari wa kwanza unaishia na neno "fahamu" basi mstari wa pili pia utaishia na silabi “mu” -Mashairi ya masivina {gum au mauve}
Haya ni mashairi yasiyofuata urari wa vina na mizani

HISIA
Hapa tunajiuliza maswali yafuatayo: -
Ni hisia zipi zinazowasilishwa na ushairi huo?

Kwa mfano; Hisia za huzuni, hisia za furaha, hisia za kukatisha tamaa, hisia za kuchekesha, hisia za kuudhi, hisia za kuogopesha au hisia za ujasiri.

Kwa ukawaida mshairi anapoandika shairi huanza yeye mwenyewe kupatwa na hisia fulani ambazo hujaribu kuzitoa kwa njia ya ushairi ili ziwasilishwe kwa hadhira.

UTENDAJI

Katika utendaji tunaangalia vipengele kama vile mtindo na utendaji. Unatendwa na mtu mmoja au watu wengi, mmoja kwa mmoja au mtu akijibizana na kundi la watu kadhaa kwa zamu.

Pia ni muhimu kuzingatia mbinu za utendaji, kama vile malighati ukariri au majibizano/ngonjera na uimbaji.
Muktadha/mazingira
Ushairi unaimbwa wapi? Wakati gani na kwa hadhira ya aina gani? Watendaji akina nani, wazee, vijana, wanawake/ wanaume

WAHUSIKA
Ushairi wa fasihi simulizi kwa kawaida ina wahusika, fanani na hadhira.
Fanani huwa wanatumika na mtunzi kufikisha ujumbe unaokusudiwa kwa hadhira.

Fanani kwa kawaida anaweza kuwa muimbaji, waghanaji n.k
Tanzu za fasihi simulizi zinatumia hadhira kama vile waitikiaji, Jukumu kubwa la waitikiaji ni kumpumzisha fanani hasa mwimbaji.

Kwa upande mwingine, ngonjera huwa na wahusika pande mbili ambapo huwa na malumbano kati yao. Dhumuni huwa ni kutoa ujumbe fulani mhusika mmoja anaweza kusema jambo moja kutoka ubeti na mwingine kulijibu jambo hili.

MATUMIZI YA LUGHA

Lugha ni malighafi ya ushairi. Lugha inayotuwa ni ile iliyokusudiwa kuinua hisia fulani kwa hadhira husika.
Matumizi ya lugha katika ushairi kuna ya aina tofauti tofauti. Uteuzi wa maneno au msamiati lazima ufuate kile unachozungumzia.

Uteuzi wa maneno(msamiati). Mambo ya kutilia maanani hapa kuhusiana na msamiati na ushairi ni: -
Matumizi ya maneno ya kale/zamani ili kuleta ulinganifu wa vina na mizani.
Uendelezaji wa msamiati ili kuwepo uhusiano wa vipindi tofauti tofauti vya kihistoria na pia kukejeli jambo au hali fulani.

 KUNA AINA MBALIMBALI ZA SEMI

Sitiari

Ni mbinu inayotumika kulinganisha vitu viwili bila kutumia viunganishi.
Kwa mfano, Mfalme ni simba

Tashihisi/uhuhishi

Kukipa kitu kisichokuwa na uhai uwezo wa kutenda kama binadamu.

Tashbiha

Ufananishaji wa kitu au jambo kwa kutumia maneno kama vile mithili ya, kama, mfano, au viunganishi

Takriri
Ni kurudia kurudia maneno, silabi, sentensi hii ni katika kusisitiza maudhui na upambaji wa lugha.
Kejeli/kinayo
Ni kumpa mtu sifa isiyofanana na jinsi alivyo.

MBINU NYINGINE ZA KISANAA.
Taswira

Haya ni maelezo ambayo hutumika kuunda picha ya kitu, hali, wazo au dhana fulani akilini mwa msomaji au msikilizaji.
Ni mbinu ambayo msanii anatumia katika kazi yake ya fasihi kwa lengo la kuwakilisha wazo, dhana ya kitu kingine
Mfano; neno “Ua” …. Huashiria mpenzi/ mwanamke mzuri(mrembo)

Tafsida

Ni kutumia lugha iliyo fasili siyo kali ili kuficha ukali au uchafu wa maneno machafu au yanayokarahisha yasitumike moja kwa moja.
Pia msanii hutumia misemo na nahau; hii ni katikaharakati za kuipamba kazi yake ya fasihi simulizi na pia katika kutajirisha maelezo yake.

Matumizi ya methali

Msanii hutumia methali katika ushairi kwa lengo la kupitishia hekima pia zinatumiwa ili kujenga kejeli kuhusu masuala tofauti tofauti ya jamii.