Kila lugha Ina asili yake. Lugha huwepo ili kukidhi haja ya mahitaji ya kimawasiliano ya jamii inayohusika
Lugha ya asili ya jamii yoyote ile hutupa picha halisi ya shughuli za maisha za jamii hiyo. Mfano shughuli za kazi, sanaa, ufundi, mila na desturi n.k
Ijapokuwa lugha ni kipengele kimojawapo cha utamaduni lakini ndicho chombo muhimu kinachotumika kuwasilisha hisia na fikra za wanajamii
Asili ya lugha ya Kiswahili ni nini?
Kuna nadharia mbalimbali zinazoelezea asili na chimbuko la lugha ya Kiswahili, nazo ni;
i. Nadharia ya asili ya Kiswahili ni kongo
ii. Kiswahili ni pijini au krioli
iii. Kiswahili ni kiarabu
iv. Kiswahili ni lugha ya vizalia
v. Kiswahili ni kibantu
Kiswahili ni kibantu
Wataalamu wa lugha za Afrika wanatambulisha lugha ya Kiswahili kuwa ni lugha mojawapo ya lugha za kibantu. Kwa msingi huo hapana budi ufafanuzi wa chimbuko na maendeleo yake ufanywe kwa kuzingatia historia ya kuzagaa kwa wabantu kusini mwa jangwa la sahara.
Neno bantu lina maana ya watu katika lugha nyingi za waafrika wanaoishi kusini mwa jangwa la sahara. Lugha za watu wanaoishi katika eneo hili huitwa lugha za kibantu
Kuna mitazamo miwili juu ya nadharia hii. Ushahidi wa kiisimu na ushahidi wa kihistoria
USHAHIDI WA KIISIMU
Huu ni mtazamo unaothibitishwa kwa misingi inayohusu sayansi ya lugha. Unadhihirisha kuwa Kiswahili ni kibantu, katika ushahidi huu wa kiisimu kuna vipengele kadhaa vinavyothibitisha kuwa Kiswahili ni kibantu.
Msamiati
Msamiati wa lugha za kibantu na Kiswahili zina mfanano mkubwa. Msamiati wa msingi ni ule unaohusu mambo ambayo haubadilikibadiliki kutokana na mabadiliko ya utamaduni. Tofauti zinaweza kujitokeza katika matamshi au mabadiliko kidogo ya viambishi vyake lakini sio mzizi. Mfano;
Kiswahili
|
kihaya
|
kijita
|
kiluguli
|
maji
|
amaizi
|
amanji
|
manzi
|
kichwa
|
omutwe
|
omutwa
|
litwi
|
macho
|
amaiso
|
ameso
|
sinenge
|
Muundo
Muundo wa sentensi za Kiswahili unafanana sana na miundo ya sentensi za kibantu. Muundo wa sentensi za Kiswahili na lugha za kibantu unachukua muundo wa kiima na kiarifu.
Mfano Kiima Kiarifu
Kiswahili: Juma anafuga kuku, mbuzi na ng’ombe
Kinyatur Juma ugufugha nkuku,mburi na ng’ombe
Kihaya: Juma nafuga unkoko ,embuzi, n’ete
Kinyakyusa: Juma ikutima nguku, imbene ni ng’ombe
Katika sentensi hizo hapo juu inaonyesha kuwa kuna mfanano kati ya sentensi ya Kiswahili na kibantu, kwani kiima kina nomino (jina) mtenda na kiarifu ambacho hufafanua tendo linaliofanywa na nomino pamoja na nomino mtendwa
Ngeli za majina
Hapa kuna makubaliano kufuatana na ngeli katika maumbo ya nomino na upatanisho wa kisarufi kati ya lugha ya Kiswahili na lugha za kibantu
Maumbo ya umoja na wingi .
Majina ya lugha za Kiswahili na lugha za kibantu yana maumbo dhahiri ya umoja na wingi. Mfano;
Kiswahili: mtu – watu
Kijita: omunu – bhanu
Kisukuma: munhu – bhanu
Kihaya: muntu – abantu
Kigezo cha upatanisho wa kisarufi
Sentensi za lugha ya Kiswahili na kibantu zina upatanisho wa kisarufi kwenye kiambishi awali cha kitenzi na nomino. Mfano;
Kiswahili: mtoto anacheza
Kijita: omwana Kenya
Kisukuma: ng’wana alibina
Kisinza: omwana na nazana
Mnyambuliko.
Mnyambuliko wa vitenzi vya Kiswahili hufanana na ule wa vitenzi vya lugha za kibantu. Mfano;
Kiswahili: Piga – kupigana, pigana, pigika
Kisukuma: Tolaga – itolagi, kivitolaga, tolekaga
Kisinza: tela – mwitele, kwitelya, teleka
Kijita: bhuma – mwibhuna, kwibhuna, bhumika
Mwanzo wa vitenzi.
Vitenzi vyote huanza na kiambishi awali cha nafsi viwe vya lugha za kibantu au Kiswahili. Mfano;
Kiswahili: Ni – nakwenada
Kisukuma: Na – leja
Kisinza: Ni – nzenda
Mwisho wa vitenzi.
Vitenzi vyote vya lugha za kibantu na lugha za Kiswahili huishia na irabu – a. mfano;
Kiswahili: nakul – a
Kihaya: nindy – a
Kisukuma: nalily – a
Kimsingi sababu zote zilizotolewa zinathibitisha kuwa kiswahili asili yake ni hapa hapa Afrika mashariki (kibantu)
USHAHIDI WA KIHISTORIA
Ushahidi wa kihistoria unathibisha kuwa lugha ya Kiswahili ilizungumzwa pwani ya Afrika mashariki, hata kabla ya ujio wa wageni kama vile waarabu na wazungu.
Ushahidi wa Al – Idris
Yasemekana uzinduzi huu ulifanywa huko sicily yapata mwaka 1100 – 1166 kwenye mahakama ya mfalme Roger II, licha ya kufahamika kuwa Kiswahili kilipata kuandikwa kabla ya 10BK Ali Idris alikuwa wa kwanza kugundua jina la zamani la Zanzibar kuwa ni unguja pia kwenye maelezo yake ameandika majina ya aina ya ndizi mbalimbali ambazo zilipatikana huko kama vile kikombe, sukari na mkono wa tembo
Ushahidi wa Ibn Batuta karne ya 14BK
Huyu ana asili ya kiarabu na alifika miji ya upwa wa Afrika mashariki mwaka 1331 BK. Katika maandishi yake anaongelea miji ya kilwa na Mogadishu na analeza maisha ya huko katika nyakati hizo’
“Basi nilianza safari toka Mogadishu kwenda nchi ya waswahili na mji wa kilwa ambao umo katika nchi ya zenji. Tulifika Mombasa kisiwa kikubwa, mwendo wa siku mbili kutoka nchi ya waswahili ” Alikuta watu hawajishunghulishi na kilimo ila huagiza nafaka kutoka kwa waswahili alikuta watu hawajishughulishi na kilimo ila huagiza nafaka kutoka kwa washahili .
Historia ya kilwa kivinje na kilwa kisiwani
Kimsingi, habari zinaelezea historia ya Kilwa karne ya 10 – 16 BK na inahusisha na kutaja majina ya utani waliokuwa wanatumia masultani wa kwanza wa kilwa. Ali Ibn Hussein na mwanaye Mohamed Ibn Ali majina hayo ni kama vile “mkoma watu” na “nguo nyingi” n.k Kutokana na habari hizi inawezekana lugha ya Kiswahili ilianza kutumika mnamo karne ya 10 – 16 BK. Na pia baada ya sultani aliyeitwa TaltIbnal Hussein ambaye alipewa jina la utani”hasha hazifiki”
Ushahidi wa Marcopolo
Ni mzungu ambaye alikuwa ana jishughulisha na maswala ya kijografia na alisafiri sehemu mbalimbali duniani. Na katika maandishi yake anasema kwamba Zanzibar ni kisiwa kizuri ambacho kina ukubwa wa mzunguko wa maili 200, watu wanamwabudu Mungu na wana mfalme wao na wanatumia lugha pia hawalipi kodi (ushuru)
Pia inasemekana ameandika kitabu cha kijografia ambacho hakikupatwa kuchapishwa lakini sehemu zake zilipata kutafsiriwa kifaransa na kirusi. Mfano; katika kitabu chake aliandika hivi
“Kisiwa cha maajabu ambacho mji wake mkuu huitwa katika lugha ya kwao Zanzibar – unguja na wakazi wake ijapokuwa ni mchanganyiko kwa sasa, wengi wao ni waislamu, chakula chao kikuu ni ndizi. Kuna aina tano za ndizi nazo ni fili, kundi mwiyani, sukari”
Ushahidi wa Al – Masudi (915 BK)
Katika maandiko yake, al masudi anazungumzia juu ya wakazi wa mwambao ambao walijulikana kwa jina la “wazanji” kwa maana hii neno Zanzibar linatokana na zanjibar yaani pwani ya “zanji” Pia anaendelea kueleza kuwa wazenji walikuwa na watawala wa kilimi ambao waliaminiwa kutawala kwa nguvu za mungu viongozi hawa pia walikuwa wacha mungu.
Inasemekana pia neno wakilimi lina maana ya “wafalme” pia anaendelea usisitiza kuwa wazenji walikuwa na kiongozi wao wakihutubia kwa lugha yao kutokana na neno zenji, kuna uwezekano kuwa kabla ya kuja kwa waarabu Kiswahili kiliitwa “kiazania” au “kizenji” na wageni walipofika pwani.
Ushairi wa Kiswahili.
edu.co.tz
Tukichunguza maandishi ya fani ya ushairi (tenzi) Kama vile utenzi wa fumolyongo ambao uliandikwa karne ya 13 BK. Kuwepo utenzi huu kunadhihirisha kuwepo kwa lugha ya Kiswahili kabla yahapo na huenda Kiswahili kilianza kutumika tangu karne ya 10 BK
Kwani Kiswahili kilichotumika katika utenzi huu ni aina ya lahaja ambayo ni ya zamani sana, kwahiyo kutokana na hayo tunaanza kudhihirisha kwa Kiswahili ni kibantu.
Maandishi ya Morice karne ya 18BK
edu.co.tz
Maandishi ya morice yalijitokeza mwaka 1776. Yeye anawagawa wakazi wa afrika mashariki katika makundi matatu “waarabu” “wasuriyama” na “waafrika” anasema kuwa wasuriyama na waafrika walikaa na kuungana kama jumuiya moja wakaoana na kusema lugha moja ya kisuriyana na inawezekana kwamba kisuriyana ndicho Kiswahili cha leo.
Utenzi wa tambuka karne ya 18 BK
edu.co.tz
Utenzi huu uliandikwa karne ya 18 kuanzia 1700 katika uchunguzi uliofanywa na dokta E.A Alpers huko Gao mji wa Panjiu ligundua barua 14 ambazo zimeandikwa kwa hati na tafsiri iliyotolewa kwa kireno. Huko ushahidi kuwa barua hizi ziliandikwa kati ya mwaka 1711 na 1725 zilitumia lugha ya lahaja ya kimvita.
LAHAJA
Ni tofauti zilizomo ndani ya lugha kuu moja ambapo watumiaji wa eneo moja hutofautiana na watumiaji wa eneo jingine
AU
Aina za lahaja
Lahaja za kijamii – ni lahaja ambazo huzuka kutokana na kuwepo kwa matabaka mbalimbali yatokanayo na tofauti za kiuchumi, kimadaraka na kisiasa. Watu wa tabaka moja huwa na lugha yao sio tu kwa ajili ya kutambulisha tabaka lao. Lahaja za kijamii zinaonekana wazi bara la ulaya kwa sababu matabaka yako wazi kabisa
Lahaja za kijografia – ni lahaja ambazo hutokana na lahaja hiyo kuzungumzwa na watu wanaoishi katika eneo moja lakini wanatengwa na kilima au kisiwa. Lahaja zote za Kiswahili ni lahaja zilizotokana na umbali wa kijografia. Lahaja hizo ni;
Kiunguja na kimakunduchi – ni lahaja ambazo zilizungumzwa katika kisiwa cha unguja na viunga vyake
Kingozi – lugha hii ilizungumzwa tangu kale huko kisimanyuna kaskazini mwa lamu. Lugha hii ilitokana na watu walioishi sehemu iliyoitwa ”ngozi” na watu hao kabila lao liliitwa wangozi pia walitumia lugha hii katika balaa kuu la nchi ya Pate (bungu na serikali ya nchi hiyo).
Kihadimu/ kitumbatu – kihadimu ambacho pia huitwa kikae au kimakunduchi kina maneno mengi ya asili ya Kiswahili. Kimsingi kitumbatu na kihadimu kinatofautiana sana na kiunguja lakini kina karibiana sana na kipemba
Kingao – kinatumika sehemu za kilwa na kuendelea kusini. Lugha hii imefanana na lugha za makabila yanayoizinguka kilwa.
Kimtang’ata – lugha hii inasemwa sehemu za mlima hasa sehemu za Tanga na Pangani na miji iliyopakana nayo. Kimkang’ata kinafanana na kimvita na kyomuu
Kiungwana – lugha hii inatumika mashariki mwa Zaire, kiungwana ni mchanganyiko wa lahaja za kienyeji na Kiswahili pamoja na Kifaransa. Chimbuko lake ni baada ya wenyeji wa pwani ya Africa mashariki kuhamia huko kongo/ Zaire
Kimrima – ni lahaja inayozungumzwa sehemu za Tanga, Pangani, Dar es salaam, Rufiji na Mafia. Kimrima kinafanana na kimtang’ata, kingao, kivumba na kiunguja kwa kiasi kikubwa
Chimbalazi/chimani– kinazungumzwa sehemu za Pwani ya Somalia, Mogadishu, mahali ambapo lugha hii inazungumzwa sana na miaka na barawa na inafanana kitukuu.
Kipemba – kinazungumzwa katika kisiwa cha Pemba pia kipemba kinachanganya maneno ya lugha mbalimbali kama vile kimvita, kitumbatu na kimtang’ata.
Kivumba – kinazungumzwa sehemu za kaskazini mwa tanga (Tanzania) na kusini mwa Kenya sehemu za vanga na wasini.
Kisiu – lugha hii husemwa kuzunguka mji wa Siu, kisiu ni lugha inayofanana sana na lugha ya kipate na kiamu.
Kiamu – lugha hii inazungumzwa katika kisiwa cha amu (Lamu) kiamu kina maneno mengi ya lugha za kibantu.
Kitukuu (kibajuru/kigunya) – vinazungumzwa kusini mwa Somali na kaskazini mwa Kenya (lamu) hadi kisimanyu. Sehemu hii ndiyo inayoitwa shungwaya na ambapo watu wanaamini kuwa chimbuko la Kiswahili kitukuu kinafanana sana na Kiswahili cha leo.
Kipate – lugha hii inasemwa katika kisiwa cha pate. Kisiwa hicho kipo kaskazini mwa pwani ya Kenya, mashariki mwa lamu
Kimvita – chimbuko la lugha hii ni kisiwa cha Mombasa, ni lugha iliyo katikati yaani matenga, lugha ya kaskazini kiamu, kisiu, kipate na kadhalika na zile za kisiu, kivumba kipemba kimtang’ata.
Kingare, kijomvu na chichifudi – chichifudi husemwa sehemu za kusini mwa gaza kati ya mji wa mkunumiji na ranisi. Kingare huzungumzwa Mombasa sehemu ya bandari ya kilindini na kijimvu kaskazini mwa Mombasa
Kimafia – kinazungumzwa sehemu za Mafia
Lahaja hizi za Kiswahili zinawezwa kugawanywa katika makundi makuu manne, ambayo ni;
Lahaja za kusini – hizi ziko visiwa vya pemba, unguja na Komoro na hujumuisha kipemba, kiunguja, kihadimu, kingazija, kitumbatu n.k
Lahaja za bara – hizi hujumuisha kiungwane na misumo ya wageni kama vile wahindi na wazungu
Lahaja za kaskazini – hizi ziko mwambao wa Somalia na Kenya. Hizi hujumuisha lahaja ndogondogo kama vile ya kiamu, kisiu, kingozi, kipate, kishale, kitukuu na chumbauzi n.k
Lahaja za katikati – hizi hujumuisha lahaja za kivumba, kimrima, kijomvu na kimtang’ata
CHANZO CHA LAHAJA
Lahaja hizi zimetokea kutokana na sababu zifuatazo;-
Utengano wa kijografia – kuna mambo mbalimbali yanayotokea na kusababisha watu wanaosema lugha moja kutengana kijografia. Wakitengana mawasiliano yao hupungua kuna uwezekano mpana wa watu walioachana kukuza upekee na usemaji kwahiyo msingi wa upekee katika usemaji ni utengano wa kijiografia (mazingira)
Kupita kwa wakati – wakati pia ni kitu muhimu kinachoweza kusababisha kuzuka kwa lahaja. Kwahiyo upekee wa usemaji hutokea taratibu kadri wakati unavyopita
Utengano wa kitabaka – kwenye jamii moja huweza kuwa na matabaka mbalimbali na kila tabaka hujitambulisha kwa namna ya pekee japokuwa matabaka hayo yapo katika eneo moja. Sababu za utengano huo waweza kuwa wa kiuchumi, kisiasa, elimu na dini kwa sababu ya muachano huo mawasiliano ya mara kwa mara kujitokea husababisha balaa na upekee wa usemaji kupanuka.
MAMBO YANAYOSABABISHA KUDHOOFIKA KWA LAHAJA
Maendeleo ya njia za usafirishaji – njia za usafirishaji kama vile barabara, meli (mitumbwi), reli n.k husababisha kudhoofika kwa lahaja kwasababu njia hizi huwakutanisha watu pamoja waliotengana kijografia. Matokeo ya kukutana huku ni kusawazisha hata namna ya kuongea
Kuwepo chini ya utawala au dini moja
Vyombo vya habari -vyombo hivyo ni kama vile redio, televisheni, magazeti husaidia katika kuunda umoja na upekee miongoni mwa watu. Umoja ni kichocheo cha ukaribiano katika usemaji.
MATUMIZI YA LAHAJA
Lahaja ina dhima (matumizi) mbalimbali katika lugha husika dhima ya lahaja katika lugha ya Kiswahili
Hukuza lugha – lugha ya Kiswahili hukua kwasababu ya kuchukua baadhi ya misamiati kutoka katika lahaja mbalimbali mfano; kivumba – kawashindi – aliwashinda, sinakuja – minakuja
Kupamba mazungumzo ya wasemaji – husaidia kupamba mazungumzo ya wazungumzaji husika kwasababu huibua misemo mbalimbali wanayoitumia katika mazungumzo yao ya kila siku.
Kusanifisha lugha – usanifishaji wa lugha unatokana na kuteuliwa kwa lahaja moja kati ya lahaja nyingi. Mfano, kiunguja kiliteuliwa kuwa lahaja ya usanifishaji miongoni mwa lahaja za Kiswahili
Kuonesha mitindo mbalimbali ya wasemaji mfano – mpemba – kipemba Zaire (kingwana) mfano Batoto bangu bana kula kingwana